Ugiriki yapendekeza kura ya maoni

Waziri Mkuu wa Ugiriki George Papandreou
Image caption Waziri Mkuu wa Ugiriki George Papandreou

Serikali ya Ugiriki inaunga mkono mpango ambao haukutarajiwa wa Waziri Mkuu George Papandreou wa kufanya kura ya maoni, kuhusu mpango wa mataifa ya bara Ulaya yanayotumia sarafu ya Euro, wa kuinusuru taifa hilo.

Katika mkutano ulioendelea hadi usiku wa manane Bwana Papandreou aliwaambia mawaziri kuwa serikali ilihitaji idhini kutoka raia wa Ugiriki.

Baraza la mawaziri limekubali hatua hiyo huko Bwana Papandreou akijitayarisha kukutana na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani kuwahakikishia kuwa kura ya maoni haitavuruga mpango huo uliokubaliwa wiki iliyopita.

Mhariri wa BBC wa maswala ya Ulaya amesema kuwa Bwana Papandreou atawaambia viongozi wengine wa bara Ulaya kuwa kura hiyo ya maoni ndio njia pekee ya kukabiliana na pingamizi ya mpango huo ambao hauungwi mkono na wengi.