Ireland yafunga ubalozi Vatican

Jamhuri ya Ireland, ambayo ni moja kati ya mataifa yenye utamaduni mzito wa kikatoliki imetangaza kuwa inafunga ubalozi wake mjini Vatican.

Waziri wa mashauri ya Kigeni wa Ireland, Eamon Gilmore, amesema wamechukua hatua hiyo kupunguza matumizi ya serikali na sio kutokana na mzozo kuhusu namna kanisa hilo linavyoshughulikia kashfa ya unyanyasaji wa watoto nchini humo.

Mwezi Julai, serikali ya Ireland ilishutumu Vatican kusaidia kuwalinda makasisi wanaohutumiwa kuwanyanyasa watoto.

Mkuu wa kanisa katoliki Ireland, Kadinali Sean Brady, alielezea kusikitishwa na uamuzi huo.