Shambulizi la kanisani, 2 wafa Nigeria

Maafisa Kaskazini mwa Nigeria wanasema kuwa watu wasiopungua wawili wameuwawa kwa kupigwa risasi na wengine kumi na moja kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa na watu waliojihami kwa bunduki dhidi ya kanisa moja.

Shambulio hilo lilitokea wakati waumini walikuwa wakikesha katika mji wa Zonkwa, jimbo la Kaduna.

Waandishi wa habari wanasema kuwa kumekuwa na hali ya wasiwasi tangu uchaguzi uliofanyika mwezi Aprili ambako jimbo hilo lilimchagua gavana wake wa kwanza ambaye ni mkristo.

Takriban waislamu 3000 ambao walilazimika kukimbia makaazi yao mwezi Aprili bado wanaishi katika kambi za muda.