Wakaguzi wa EU na IMF kuzuru Ugiriki

Maafisa wa ngazi ya juu katika muungano wa ulaya EU na waakilishi wa shirika la fedha duniani, IMF, wanatarajiwa nchini Ureno ambako watakagua juhudi zilizopigwa na nchi hiyo katika kutekeleza makubaliano ya muungano wa ulaya ili iweze kupokea mkopo wa euro bilioni 78.

Serikali ya Ugiriki imeshurutishwa na EU kupunguza matumizi ya umma kabla ya kupokea fedha hizo.