Kashfa ya ngono yamtatiza mgombea urais

Mwanasiasa mashuhuri anayegombea tiketi ya urais ya chama cha Republicans nchini Marekani, amekanusha madai mapya kuwa alijaribu kumlazimisha mwanamke mmoja kufanya mapenzi naye.

Herman Cain anaongoza wanaogombea tiketi hiyo ilikukabiliana na Rais Barack Obama kwenye uchaguzi mwakani.

Akizungumza kwenye runinga ya ABC, Bw Cain amesema madai hayo ni ya uongo na atayajibu ipasavyo katika mkutano na waandishi wa habari leo jumanne.

Bi Sharon Bialek, ndiye mwanamke wa kwanza kujitokeza hadharani kudai kuwa Bw Cain, alijaribu kufanya mapenzi naye kwa lazima miaka kumi na minne iliyopita wakati akitafuta kazi.

Huyo ni mwanamke wa nne kutoa madai hayo na maswali kuhusu tabia ya mwanasiasa huyo huenda yakaathiri mikakati yake ya kugombea urais