Wanamgambo 70 wauawa Afghanistan.

Mapigano makali yametokea kati ya wanajeshi wa Muungano wa NATO na wapiganaji wa waasi Kusini Mashariki mwa Afghanistan, baada ya wanamgambo hao kushambulia kituo kimoja cha kijeshi karibu na mpaka wa Pakistan.

Afisa mmoja wa serikali ya Afghanistan, amesema kati ya wanamgambo 60 na 70 waliuawa kwenye makabiliano hayo.

Jeshi la NATO liliitisha msaada wa wanajeshi wa angani ili kuwatawanya wapiganaji hao wa waasi ambao walikuwa wamejihami na silaha nzito nzito.

Hakuna mwanajeshi yeyote wa NATO au raia aliuawa wakati wa mapigano hayo yaliyotokea katika mkoa wa Patika.

Maafisa wa idara ya ujasusi nchini Afghanistan, wanasema waasi hao wanatoka kundi ya wapiganaji wa Haqqani na waliingia nchini humo kutoka Pakistan.