Msafara kutoka Libya umekamatwa Niger

Ripoti kutoka Niger, zinasema kuwa jeshi la nchi hiyo limenasa msafara wa magari ambayo yalikuwa yakitoka nchini Libya kuelekea Mali.

Jeshi la nchi hiyo pia lilinasa shehena kubwa ya silaha kutoka kwa msafara huo.

Haijulikani wazi ni nani alikuwa kwenye msafara huo, lakini msafara huo ulitumia barabara iliyotumika na aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi nchini Libya wakati wa utawala wa Kanali Gaddafi Abdullah al-Senuss mwezi uliopita.

Al-Senuss anaaminika kujificha nchini Mali.

Baadhi ya silaha zilizonaswa ni pamoja na bunduki za rashasha, gruneti zinazorushwa kwa makombora na risasi.