Mashirika yatoa wito wa msaada zaidi

Mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yamesema kuwa yanakabiliwa na uhaba wa pesa za kuendesha shughuli za kuwasaidia watu walioathirika na mafuriko yaliyoathiri pakubwa maeneo ya Kusini mwa Pakistan mapema mwaka huu.

Mashirika hayo yanasema kuwa ikiwa yatashindwa kukusanya fedha za kutosha, mamilioni ya raia wa taifa hilo watabaki bila chakula na makao.

Shirika la Save the Children, limesema limefanikiwa kukusanya thuluthi moja pekee ya msaada unaohitajika katika bajeti yake wakati shirika la Care International nalo likiripoti kuwa na upungufu wa asilimia 91 katika bajeti yake.

Shirika la Oxfam linasema uhaba huo utalazimisha kiwango cha msaada kupunguzwa baada ya mwezi ujao.