Huduma za simu zaimarika barani Afrika

Ripoti mpya imebaianisha kuwa bara la Afrika sasa ndilo soko la pili kwa ukubwa duniani la simu ya mkononi baada ya bara la Asia.

Ripoti hiyo imenadi kuwa utumizi wa simu unakua kwa kiasi kikubwa barani Afrika, kuliko sehemu nyingine duniani.

Inakadiriwa kuwa bara la Afrika lina zaidi ya watumizi wa simu milioni 650.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, iliyotayarishwa na chama cha makampuni zinazotoa huduma za simu, GSM Association, Nigeria inaongoza barani Afrika na idadi kubwa ya watu wanaotumia simu za mkononi.