Uzalishaji wa mafuta umepungua Sudan

Serikali ya Sudan Kusini, imesema kuwa uzalishaji wa mafuta ghafi umepungua kwa asilimia 25 tangu taifa hilo lilipojinyakulia uhuru wake miezi minne iliyopita.

Waziri katika serikali ya Sudan Kusini, amesema wahandisi wengi kutoka Sudan waliondoka kutoka maeneo ya kuchimba mafuta, baada nchi hiyo kuanza kujitawala na kwa sasa kuna upungufu wa wafanyakazi wenye ujuzi na waliohitimu.

Msimu wa mvua pia unafanya shughuli ya kukarabati vifaa vilivyoharibika na barabara katika sehemu zinazozalisha mafuta, katika jimbo la Unity kuwa ngumu.

Kuna ripoti kuwa makundi ya waasi yanaendelea na shughuli ya kuchimba mafuta kinyume cha sheria.

Serikali ya Sudan Kusini, hupata asilimia 98 ya mapato yake yote kutokana na uuzaji wa mafuta.