Viongozi wa Upinzani washumbuliwa Misri

Wanaharakati wa kijamii kutoka Syria na Misri wamewazuia viongozi wa upinzani kutoka Syria, kukutana na viongozi wa jumuiya ya nchi za Kiarabu mjini Cairo wakiwashutumu kwa kueneza uongo.

Wanaharakati hao waliwarushia mayai na kukabiliana na viongozi hao wa upinzani walipowasili katika makao makuu ya Jumuiya hiyo mjini humo.

Waandishi wa habari wanasema tukio hilo, limeonyesha mgawanyiko mkubwa ndani ya vugu vugu linalopinga serikali nchini Syria.

Viongozi hao wa upinzani wametajwa kama watu ambao hawana maana yoyote kwa raia wa Syria na watu ambao kamwe hawawezi kutambua kinachotendeka kwa sasa.

Mkutano huo wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu umehairisha.