Wanjeshi wakomboa meli iliyotekwa nyara

Runinga ya taifa nchini Ugiriki imesema kuwa wanajeshi wa nchi hiyo wamekomboa meli moja iliyokuwa na zaidi ya abiria ishirini iliyotekwa nyara jana usiku.

Ripoti hiyo imesema kuwa maafisa wa kitengo maalum cha jeshi la nchi hiyo walivamia meli hiyo na kumpiga risasi na kumuua mmoja wa watekaji nyara hao.

Awali naodha wa meli hiyo aliliambia shirika hilo la habari la ataifa kuwa meli hiyo ilikuwa imetekwa nyara na waasi wa kikurdi.