Arroyo kwenda ngambo matibabu

Mahakama kuu nchini Ufilipino imempa aliyekuwa rais wa nchi hiyo , Gloria Arroyo, ruhusa kusafiri nje ya nchi.

Uamuzi huo wa mahakama ni kinyume na uamuzi uliotolewa na mrithi wake ambaye ni rais wa sasa Benigno Aquino.

Rais huyo aliamuru Bi Arroyo asiondoke nchini humo kwa sababu anahofia huenda asirudi nchini humo kukabiliana na madai ya ufisadi yanayomkabili.

Gloria Arroyo alikuwa ameomba ruhusu kusafiri ngambo ili apate matibabu ya maradhi ya mifupa. Baada ya kunyimwa idhini aliwasilisha ombi lake katika Mahakama Kuu na majaji wanane dhidi ya watano wakapiga kura kukubali ombi lake.