Obama kuongeza wanajeshi Uchina

Rais Barack Obama ametangaza kuimarisha kikosi cha Marekani kilichopo nchini Australia kufuatia hofu inayoendelea katika kanda hiyo ya Uchina.

Katika ziara yake nchini rais Obama alisema takriban wanamaji mia mbili na hammsini watatumwa kaskazini mwa nchi hiyo kuanzia mwaka ujao.

Alisema kupelekwa kwa kikosi hicho kutasaidia kuimarisha usalama baada ya matukio ya uvurugaji usalama kiusalama na kibinadamu yaliyotokea katika eneo hilo .

Waziri mkuu wa Australia Julia Gillard, amesema kuwa kikosi cha askari elfu mbili na mia tano cha Marekani , wakiwemo wanamaji watakwenda huko .