Mwanariadha wa Kenya akatwa miguu

Mwanariadha wa masafa marefu kutoka Kenya aliyekuwa ametoweka wakati kimbunga cha baridi kali kilipokumba jimbo la Alaska amekatwa miguu yake baada ya kuathirika na maradhi ya jalidi.

Maradhi haya yanatokana na misuli ya mwili kuganda kutokana na baridi kali.

Mwanariadha huyo Marko Cheseto alikuwa amepotea kutoka chuo kikuu cha Alaska kwa siku mbili kabla ya kupatikana nje ya hoteli moja akiwa amevaa suruali ndefu aina ya jeans,jaketi na viatu vya riadha.

Cheseto ambaye amekuwa akisomea uuguzi mjini Anchorage alisema alikuwa akipitia wakati mgumu kibinafsi na amewashukuru wasamaria wema waliompata