Afrika Kusini 'kupitisha' muswada tata

Bunge la Afrika Kusini linatarajiwa kupitisha muswada wenye utata juu ya kulinda taarifa za siri za serikali hii leo.

Muswada huo utawaweka pabaya waandishi wa habari kwa kuwa mwandishi anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 15 gerezani kwa kuchapisha taarifa za siri.

Muswada huo umeshutumiwa na watu mbali mbali mashuhuri pamoja na washirika wa chama tawala ANC, chama kikuu cha wafanyakazi COSATU wakiutaja kuwa una nia ya kuwanyima uhuru waandishi na kuwatisha maafisa wanaofichua kashfa ndani ya taasisi za serikali.