Rais Saleh wa Yemen kuachia ngazi

Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh amekubali kujiuzulu wadhifa huo na kumkabadhi mamlaka naibu wake.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo anadai upinzani na upande wa serikali wameafikiana mkataba utakaomlazimu Rais Saleh kuondoka mamlakani na kuruhusu kubuniwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa.

Rais huyo ambaye anatarajiwa kutia saini mkataba huo baadaye Jumanne amekabiliwa na maandamano ya kumpinga na maasi ya koo zilizo na silaha zinazompinga.

Katika siku zilizopita alikaribia kusaini mkataba huu mara kadhaa lakini kubadili nia yake nyakati za mwisho.