Visa vya unyanyasaji Bahrain

Nchini Bahrain ripoti ya uchunguzi kuhusu ghasia na unyanyasaji dhidi ya waandamanaji wanaotaka demokrasia inatarajiwa kutolewa leo.

Ripoti hiyo itakayotolewa na tume huru ya Uchunguzi ya Bahrain, inatarajiwa kuikosoa vikali serikali .

Maafisa wa serikali tayari wamekiri kuwa wanajeshi walitumia nguvu kupita kiasi walipokuwa wakizuia maandamano ya upinzani yaliyoanza mwezi Februari mwaka huu.

Waumini wa Kiislam wa madhehebu ya Shia walio wengi watakuwa makini kuangalia ni vipi watawala wa kifalme wa madhehebu ya Suni watashughulikia ripoti hiyo.