Waandamanji wasalia Tahrir

Ahadi ya kurejesha utawala wa Misri kwa raia haraka iwezekanavyo imeshindwa kuwashawishi waandamanaji ambao wamesalia katika medani ya Tahrir katika mji mkuu wa Cairo.

Kiongozi wa baraza la utawala wa kijeshi, Field Marshal Mohamed Hussein Tantawi, akizungumza katika hotuba kwa taifa kupitia televisheni, amesema kuwa uchaguzi wa ubunge utafanyika wiki ijayo kama ilivyokuwa imepangwa na uchaguzi wa urais kufanyika mwezi Julai mwaka ujao.

Lakini waandamanaji hao wanasema kuwa ahadi hizo hazitoshi. Makabiliano kati ya waandamanaji hao na polisi yaliendelea usiku kucha.