Maafisa wa jeshi Misri waomba msamaha

Maafisa wawili waandamizi wa jeshi la Misri wameomba radhi kufuatia mauaji ya waandamanaji yanayoendelea katika mji mkuu Cairo na miji mingine nchini humo.

Majenerali hao wamejitokeza katika televisheni ya serikali wakitoa salaam za rambirambi kwa wananchi wa Misri.

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi wa baraza tawala la kijeshi kuomba radhi tangu mgogoro uanze nchini Misri.

Serikali itatangaza leo namna wanavyopanga kuendelea na shughuli za uchaguzi unaotarajiwa kuanza Jumatatu ijayo.