Viongozi wa Fatah na Hamas wakutana

Viongozi wa vyama viwili vya Kipalestina vya Fatah na Hamas wanakutana mjini Cairo kujaribu kukubaliana kuhusu kuwa na mkataba wa umoja.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ambaye anatoka chama cha Fatah anafanya mazungumzo na kiongozi wa kisiasa wa Hamas Khaled Meshaal.

Makubaliano yaliyopita kati ya pande mbili hizo yalitiwa saini mwezi Mei lakini yakashindwa kutekelezeka.

Fatah, ambao wako madarakani katika Ukingo wa magharibi wa mto Jordan na Hamas wanaotawala Gaza, wamekuwa na mgawanyiko mkubwa kwa zaidi ya miaka mitano.