Watu wapatao wanne wauawa Yemen

Habari kutoka Yemen zinasema watu wapatao wanne wameuawa wakati wa maandamano mapya katika mji mkuu, Sanaa, licha ya makubaliano yaliyofikiwa jana ambapo Rais Ali Abdullah Saleh hatimaye amekubali kukabidhi madaraka.

Mkataba huo unamhakikishia kutoshitakiwa kwa makosa anayotuhumiwa kutenda akiwa madarakani.