Morocco kuwachagua wabunge wapya

Shughuli ya kupiga kura imeanza nchini Morocco ambapo taifa hilo linachagua bunge jipya.

Uchaguzi wa leo ni wa kwanza tangu kuidhinishwa kwa katiba mpya iliyopendekezwa na Mfalme Mohamed wakati nchi za kiarabu zikishuhudia maaandamano kutaka mageuzi ya utawala.

Baadhi ya wanaharakati wa mageuzi wamepuzilia mbali mageuzi hayo na wameomba raia kususia kura ya leo.

Ushindani ni kati ya chama cha kiisilamu kilicho na mismamo wa kadri na mrengo unaounga mkono utawala wa kifalme.