Majeshi zaidi yaasi serikali ya Syria

Askari zaidi wa Syria wameshuhudiwa wakiasi jeshi la serikali na kujiunga na majeshi ya upinzani.

Mwandishi wa BBC ambaye amepenya nchini Syria ameona kundi dogo la askari ambao wamekuwa wakiasi kutoka majeshi ya usalama.

Mwandishi wa BBC amesema askari waasi wamefika mji wa Homs- ambao ni kitovu cha upinzani dhidi ya serikali, na wamemwaambia kuwa wamejiunga na upinzani baada ya kuamriwa wawafyatulie risasi waandamanaji.

Muda uliotolewa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu kwa Syria kuruhusu ujumbe wa kuchunguza hali ilivyo nchini humo unakaribia kumalizika.

Na kama Syria itashindwa kutekeleza agizo la jumuiya hiyo itakabiliwa na vikwazo.