Wanajeshi 4 wauawa Somalia

Mshambuliaji wa kujitolea mhanga ameshambulia maeneo yanayodhibitiwa na serikali katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kuwauwa wanajeshi wanne na kujeruhi wengine wengi.

Mkuu wa jeshi la Somalia Generali Abdikarim Yusuf, anaripotiwa kuponea chupuchupu.

Amewaambia waandishi wa habari kuwa mshambuliaji huyo alifanya mashambulio wakati wanajeshi wanaoshika doria wakipokezana zamu.

Haijafahamika mshambuliaji alitoka kundi gani, lakini mji wa Mogadishu umekuwa ukikumbwa na mashambulio ya mabomu yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wa kiislam wa Alshaabab.