Ghasia zapamba moto Misri

Miedani ya Tahrir Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waandamanaji katika medani ya Tahrir

Utawala wa kijeshi wa Misri unakabiliwa na shinikizo za kimataifa ukitakiwa kumaliza ghasia zinazoendelea jijini Cairo dhidi ya wanaharakati wanaoupinga utawala huo.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amewataka watawala hao kusitisha matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji, na akatoa wito ufanyika uchunguzi huru juu ya ghasia hizo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Heague ameelezea hofu juu ya taarifa za matumizi ya gesi zinazodhuru dhidi ya waandamanaji.

Ghasia zinaendelea katika medani ya Tahrir na maeneo yanayozingira medani hiyo.