Amnesty lataka G Bush akamatwe Afrika

Shirika la kimataifa la Amnesty International limetoa wito wa kukamatwa kwa aliyekuwa rais wa Marekani George W Bush katika ziara yake barani Afrika.

Bw Bush anatembelea barani humo katika nchi za Ethiopia, Tanzania na Zambia.

Nia ya ziara hiyo ni kuongeza jitihada za kupambana na saratani ya kizazi na matiti.

Shirika hilo la Amnesty limesema nchi hizo za Afrika zina wajibu wa kumkamata kulingana na sheria za kimataifa dhidi ya utesaji.