Aliyebakwa ajifungua mtoto wa mwanzo

Mwanamke mmoja wa Pakistan, aliyepata umaarufu kwa kampeni zake za kuwatetea wanawake waliobakwa, amejifungua mtoto wake wa mwanzo.

Mukhtar Mai alibakwa na kundi la watu miaka tisa iliyopita kwa amri ya baraza la wazee la vijiji.

Ilikuwa ni adhabu kwa madai kuwa kaka yake alikuwa na uhusianio nje ya ndoa.

Alichukua hatua ambayo si ya kawaida ya kuzungumza hadharani juu ya ubakaji huo na kuwafikisha wale waliombaka mahakamani, jambo lililomfanya awe mfano wa kitaifa.