Aliyegundua virusi vya ukimwi alalamika

Kirusi cha HIV Haki miliki ya picha
Image caption Umbo la kirusi cha HIV

Mwanasayansi mshindi wa nishani ya Nobel ambaye alisaidia kugundua virusi vya Ukimwi mwaka 1983 amepinga hatua ya kupunguza fedha za kukabiliana na virusi vya Ukimwi.

Mwanasayansi huyo Profesa Francoise Barré Sinoussi alitunukiwa nishani ya Dawa miaka mitatu iliyopita.

''Haikubaliki kuona baadhi ya nchi zinashindwa kutekeleza ahadi zao za kuimarisha mifuko ya kupambana na virusi vya Ukimwi'', Alisema Profesa Sinoussi katika mahojiano na BBC.

Pia amelaani mpango wa taasisi za kimataifa kupunguza au kusitisha kabisa utoaji wa fedha kwa mataifa masikini.