Muungano wa Ulaya wakosolewa vikali!

Pesa taslim za euro Haki miliki ya picha PA
Image caption Pesa taslim za euro

Waziri wa fedha wa Afrika kusini Pravin Gordhan na mwenzake wa Nigeria Ngozi Okonjo-Iweala wamesema mzozo wa madeni wa Ulaya unatishia maendeleo ya uchumi ya Afrika.

Bwn.Gordhan amesema matatizo ya kifedha ya Ulaya yanadhoofisha biashara duniani.

Bi Okonjo-Iweala amesema kuwa Muungano wa Ulaya unaweza kujifunza kutoka mataifa yanayoendelea duniani, namna ya kukabiliana na madeni, na kuendeleza ukuaji wa uchumi.

'Uchumi wa Afrika uliathiriwa mwaka 2008 na historia inajirudia' bwana Gordhan aliiambia BBC.