China yahofia soko la bidhaa zake

Serikali ya China imeonya kuwa inakabiliwa na hali ngumu ya mauzo ya bidhaa zake nje ambayo huenda isiwe nzuri mwaka ujao.

Wizara inayoshughulika na masuala ya biashara katika mataifa ya nje imetoa taarifa yake ya mwaka inayosema kuwa nchi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa kufuatia mdororo wa uchumi katika bara Uropa na Marekani inakouza asilimia kubwa ya bidhaa zake.

China inategemea sana mauzo ya bidhaa zake nje huku takriban watu milioni 80 wakitegemea mauzo hayo kujiambulia riziki.