Watoto 170 waokolewa China

Polisi nchini China wameokoa watoto 170 kutoka kwa walanguzi baada ya kuwatia nguvuni zaidi ya watu mia sita mwezi uliopita.

Maafisa 5000 katika mikoa kumi walihusika kwenye msako huo.

Taarifa zinasema kuwa sheria ya China inayolazimisha watu kupata mtoto mmoja pamoja na sheria hafifu za kupanga watoto zimechangia kuwepo kwa soko haramu.

Wizara ya usalama wa umma imesema iligundua kuhusu ulanguzi wa watoto mwezi Mei baada ya kutokea kwa ajali ya barabarani Kusini Magharibi mwa mkoa wa Sichuan.