Maafa Kusini mwa Sudan

Watu 41 wameuawa kufuatia shambulio katika jimbo la Jonglei, Sudan kusini.

Eneo hilo ni maarufu kwa mapigano ya kikabila na wizi wa mifugo.

Gavana wa jimbo la Jonglei Kuol Manyang aliiambia BBC kuwa mtoto mmoja aliuawa kwa kukatwa kwa panga.

Wengine waliteketezwa moto walipojaribu kujificha ndani ya nyumba zao.

Swala la usalama ndilo sugu zaidi katika taifa la Sudan Kusini ambalo lilijipatia uhuru wake mwezi wa Julai mwaka huu.