Rais wa Syria asema hana majuto

Rais wa Syria Bashar al-Assad amesema hana majuto kuhusu mashambulio yaliyofanywa na wanajeshi dhidi ya waandamanaji japo anaomba radhi kutokana na vifo vilivyotokea.

Katika mahojiano na televisheni ya Marekani ya ABC amesema wanajeshi hawakupewa amri ya kuua au kuwa wakatili.

Rais Assad amesema majeshi ni ya serikali na wala sio yake na kuwa alifanya kila juhudi kulinda watu wake.

Wakati huo huo Rais Assad amelaani ripoti ya Umoja wa mataifa inayodai kuwa Syria imetekeleza uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuwanyanyasa waandamanaji.

Amesema Umoja wa mataifa haujamuonyesha ushahidi kuwa uhalifu huo ulitekelezwa.