Nigeria yakatiza mawasiliano

Polisi nchini Nigeria wamesababisha usafiri kuwa mgumu kupitia daraja muhimu linalounganisha Kaskazini na Kusini mwa Nigeria ili kuzuia wapiganaji kutoka Niger Delta kusafiri hadi mji mkuu Abuja.

Takriban wapiganaji 200 wanataka kuwasilisha malalamiko yao kwa rais Goodluck Jonathan kwamba pesa wanazodai zilipwe kabla ya siku kuu ya Krismasi.

Waliahidiwa pesa hizo na serikali wakati serikali ilipotangaza msamaha kwa waasi wakati wa mashauriano mwaka 2009. Kwa sasa kuna msafara mkubwa wa magari kwenye daraja hilo katika mto wa Niger.