Maafa kwenye mkasa wa moto India

Zaidi ya watu sabini wamefariki dunia katika mkasa wa moto mkubwa uliotokea katika hospitali moja mjini Calcutta, India.

Wanaotoa huduma za dharura waliwasili katika eneo hilo na kulazimika kuvunja vioo na kutumia kamba kuwaokoa wagonjwa waliokwama katika ghorofa za juu za hospitali hiyo.

Iliwachukua saa kadhaa kuuzima moto huo unaoaminika kuanzia katika ghorofa ya chini ya jengo hilo.

Uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo umeanzishwa.