Ban Ki Moon awasili Somalia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amewasili mjini Mogadishu, Somalia.

Bw Ban anatarajiwa kukutana na viongozi mbali mbali ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa majeshi ya kulinda amani ya muungano wa Afrika yanahohudumu nchini humo.

Kulingana na Katibu Mkuu huyo, shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya kisiasa itahamishwa kutoka Kenya hadi Mogadishu mwezi wa Januari.

Kuna ulinzi mkali mjini Mogadishu huku barabara nyingi zikifungwa. Hakuna ndege zinazotua au kuondoka katika uwanja wa ndege mjini Mogadishu kwa sababu za kiusalama.

Ziara yake imejiri siku moja baada ya mapigano makali kutokea kati ya wapiganaji wa kundi la al Shabaab na walinda amani wa Muungano wa Afrika.