Madaktari Kenya warejelea mgomo

Madakatari wa hospitali za umma nchini Kenya wametupilia mbali mkataba uliotiwa saini hapo jana jioni wa kurejea kazini na kuendelea na mgomo wao hii leo.

Mwenyekiti wa chama cha madktari Dkt Victor Ng'ani alisema matatizo ya madkatari hayajashughulikiwa.

Madaktari nchini humo wanadai nyongeza ya asilimia 300 pamoja na kuimarishwa kwa mazingira ya utendaji kazi.

Mgomo huo wa madaktari umeendelea kwa zaidi ya wiki moja.