Morocco yabana wavuvi wa ulaya

Morocco imepiga marufuku maboti ya uvuvi ya muungano wa ulaya kufanya shughuli za uvuvi katika maji yake, baada ya bunge la muungano wa Ulaya kuamua kutoendeleza mkataba wa uvuvi na nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Wizara ya mambo ya nje pia imeonya kuwa huenda wakaangalia upya ushirikiano mzima baina yake na Muungano wa Ulaya.

Bunge la Muungano wa Ulaya lilikataa makubaliano hayo kutokana na hofu juu ya sheria ya eneo la sahara magharibi .

Morocco ilichukua eneo hilo mwaka 1976, lakini hatua hiyo ya serikali ya Rabat bado haijatambuliwa kimataifa.