Putin afanya mahojiano ya televisheni

Waziri mkuu wa Urusi , Vladimir Putin, anafanya mahojiano yake ya mwaka ya moja kwa moja kupitia Televisheni, ambapo hujibu maswali ya watazamaji na kuahidi kutatua baadhi ya matatizo yanayowakabili.

Lakini mahojiano ya mwaka huu yanafanyika katika hali tofauti kabisa . Katika uchaguzi wa ubunge mapema mwezi huu chama cha bwana Putin kilipoteza sehemu ya kura zake.

Maelfu ya raia wa Urusi wameshiriki maandamano ya mitaani dhidi ya kile walichosema ni wizi wa kura.

Mwandishi wa BBC mjini Moscow anasema Putin anatarajia mahojiano hayo yatasafisha jina lake kama kiongozi anayetarajiwa kugombea uirais katika uchaguzi ujao.