Uingereza washambulia mamlaka ya Kodi

Kamati ya Bunge nchini Uingereza imekosoa mipango legevu ya kodi kati ya Mamlaka ya Mapato na Ushuru (HMRC) na makampuni makubwa ya biashara.

Wabunge hao walimtaja Dave Hartnett, katibu mkuu wa masuala ya kodi kwa kushindwa kusimamia vizuri majadiliano ya kulipa kodi na baadhi ya makampuni makubwa.

Kamati ya Hesabu za Serikali ilisema makampuni makubwa yalipata upendeleo na kulikuwa na uwajibikaji mdogo kwa umma kuhusu mipango ya ulipaji kodi ilivyokuwa ikifikiwa.

HMRC imekanusha matokeo ya utafiti huo na kusema wabunge hawakuzielewa taarifa zilizopo.

Msemaji wa Waziri mkuu pia amekanusha madai kuwa kuna uhusiano wa kificho na legevu’ wa ulipaji kodi kwa makampuni hayo