Maafisa wa Usalama waa DRC walaumiwa

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linasema kuwa maafisa wa usalama katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo wameua raia 24 katika harakati za kuwasaka wanaharakati wa upinzani tangu matokeo ya uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata kutangazwa.

Ripoti hiyo imezingatia ushahidi kutoka kwa watu walioshuhudia wakiwemo jamaa za waliouawa.

Kulingana na shirika hilo, kulitokea mauaji karibu 20 kwa kipindi cha siku sita yakilenga wafuasi wa upinzani hasa katika mji wa Kinshasa.

Baadhi ya wale waliouawa ni kijana mmoja mwenye umri wa miaka kumi na tatu ambaye alikuwa nje ya nyumba yao.