Waangalizi Kuzuru Syria Leo

Waangalizi kutoka Jumuiya ya nchi za Kiarabu wanatarajiwa kuwasili nchini Syria leo kuanza mpango wa kumaliza machafuko ambayo Umoja wa Mataifa unaamini yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 5000 tangu maandamano dhidi ya serikali kuanza mwezi Machi.

Machafuko hayo yamesababisha umwagikaji damu mkubwa hasa katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo ambapo upinzani unadai kuwa takriban watu 250 waliuwa siku ya Jumatatu na Jumanne.

Serikali inasisitiza kuwa inapigana dhidi ya makundi ya kigaidi. Katika taarifa moja kali kuhusu Syria, Marekani ilisema kuwa rais Bashar al-Assad amepoteza uhalali wake.