Sudan Kusini yazuia uzalishaji wa mafuta

Serikali ya Sudan Kusini imesema inasitisha kutoa mafuta yake kutokana na mgogoro unaozidi kuendeleea na upande wa Sudan kusini kuhusu ushuru.

Waziri wa habari wa Sudan Kusini Barnaba Benjamin ameiambia BBC kuwa hatua hiyo ya kusitisha utoaji huo wa mafuta utachukua wiki mbili.

Mafuta mengi ya Sudan yako Sudan Kusini lakini huhitaji bomba la Sudan Kaskazini kusafirisha mafuta yake.

Nchi hizo mbili zinazozana juu ya malipo ya matumizi ya bomba hilo.