Mwingereza ashtakiwa kwa ugaidi Kenya

Raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 29 anayekabiliwa na mashtaka ya ugaidi nchini Kenya amekana mashtaka yote yanayomkabili.

Jermaine Grant na wenzake watatu ambao ni raia wa Kenya wamekana mashtaka hayo.

Wanashtakiwa pia kwa kupatikana na bidhaa zinazotumika kutengeneza vilipuzi kwa nia ya kutenda uhalifu.

Bw Grant tayari amepewa kifungo cha miaka mitatu kwa kupatikana na hatia ya kuwa nchini Kenya kinyume cha sheria na kutoa habari za uongo.