Polisi UK yachunguza madai ya Walibya

Polisi wa Uingereza wanatarajiwa kuchunguza madai kuwa mashirika ya kijasusi nchini humo yalisaidia katika kuwahamisha washukiwa kisiri huko Libya.

Walibya wawili walioshiriki katika kupinga uongozi wa Kanali Gaddafi wanatishia kuishtaki Uingereza kwa kuhamishiwa Libya na kuteswa.

Utafiti huu mpya unaweza kuchelewesha uchunguzi wa serikali juu ya washukiwa wanaohamishwa kisiri.

Polisi na waendesha mashtaka wa Uingereza wamesema maafisa wa mashirika ya kijasusi ya Uingereza M15 na M16 hawatoshtakiwa kwa madai tofauti ya njama za utesaji.