Hague: Mabadiliko Burma yainaridhisha

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza , William Hague, ameonya dhidi ya kulegezwa kwa masharti yaliyowekewa serikali inayoungwa mkono na jeshi nchini Burma.

Hague anayekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini humo amefanya mashauriano na serikali na upinzani, na kusema ana imani katika mwelekeo ya mabadiliko nchini humo.

Hata hivyo amesema kuwa serikali hiyo inapaswa kuonyesha jitihada zaidi kabla ya kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekewa nchi hiyo.