Elfu 3 waliuawa wiki jana Sudan Kusini

Takriban watu elfu tatu wanadaiwa kuuawa nchini Sudan Kusini katika machafuko mabaya ya kimbari yaliyotokea wiki jana.

Haya ni kwa mjibu wa afisa mkuu wa eneo la Pibor, jimbo la Jonglei, Joshua Konyi.

Ameambia vyombo vya habari vya kigeni kwamba miili ya wathirika imetapakaa kote katika eneo hilo.

Wapiganaji wa kabila la Murle na wale wa kabila la Lou Nuer wametekeleza wizi wa mifugo na mashambulio ya kulipiza kisasi katika kipindi cha mwezi mmoja yaliyosababiha vifo vya zaidi ya wa elfu moja.