Mlipuko waua kadhaa Syria

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua mjini Damascus, imesema televisheni ya taifa ya Syria.

Imesema watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika mlipuko huo katika wilaya ya Midan.

Shambulio hili linakuja wiki mbili baada ya watu 44 kufa katika milipuko ambayo mamlaka zimedai imefanywa na magaidi.

Wilaya ya Midan imekuwa eneo ambalo maandamano ya hivi karibuni ya kupinga serikali ya Rais Bashar al-Assad yakifanyika.