Aliyekuwa mkuu wa jeshi akamatwa Uturuki

Aliyekuwa mkuu wa jeshi nchini Uturuki amekamatwa katika uchunguzi wa madai ya jaribio la kuipindua serikali.

Mwendesha mashtaka anataka Generali Ilker Basbug azuiliwe baada ya kutoa ushahidi kwa saa kdhaa katika mahakama ya Istanbul.

General Basbug ndiye afisa wa ngazi ya juu zaidi kuhusishwa na kundi ambalo lilikua limepanga njama ya kupindia serikali ya Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan.